Blog hii inahusu taarifa mbali mbali za kisiasa,michezo,elimu,technolojia na matangazo mbali mbali ya biashara
Jumatano, 26 Oktoba 2016
Jumamosi, 1 Oktoba 2016
MANENO YA UTANI YA ZITTO KABWE KUSHANGILIA GOLI LA MKONO LA YANGA
October 1,kulichezwa mechi ya watani wa jadi kati Simba na Yanga na timu hizo kutoka sare ya kufungana mabao 1-1. Kufuatia goli la Yanga lililofungwa na mchezaji Hamis Tambwe kusemekana limefungwa kwa mkono, mh. Zitto Kabwe akatumia account yake ya twitter kumwandikia Freeman Mbowe ambaye ni mshabiki wa Yanga "Mwenyekiti wangu Freeman Aikael Mbowe umetambua goli la mkono lakin umeshindwa kumtambua Lipumba km mwenyekiti CUF".
MECHI YA WATANI WA JADI
Mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga imemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 1-1. Yanga ilikuwa timu ya kwanza kujipatia bao lake la kuongoza dakika ya 26 ya mchezo kupitia mchezaji wake mahiri Hamis Tambwe.Bao hilo lilileta vurugu kwa mashabiki wa Simba hadi kupelekea kung'oa viti na kuvitupa uwanjani,,,katika vurugu hizo ilipekea mchezaji nahodha wa Simba Jonas Mkude kupigwa kadi nyekundu. Simba iliendelea kucheza ikiwa pungufu hadi dakika ya 87 ya mchezo,mshambuliaji Kichuya wa Simba alivyosawazishia timu yake kwa goli safi la mpira wa kona ulioingia moja kwa moja wavuni na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)







